Taswira ya Jamii ya Kisasa kwa Mujibu wa Riwaya Teule za Kisasa za Mwandishi K.W. Wamitila
DOI:
https://doi.org/10.47604/ijl.1538Keywords:
taswira ya kisasa, jamii ya kisasa, usasaleo, riwaya mpyaAbstract
Lengo: Makala hii inakusudia kuangazia taswira kamili ya jamii ya kisasa kama ilivyodhihirika katika riwaya mpya teule za Musaleo! na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji zilizoandikwa na K.W. Wamitila. Mwandishi amefanikiwa kuieleza jamii ya kisasa kupitia kwa usimulizi wenye simulizi nyingi fupi fupi ambayo ni kipengee kimojawapo cha mbinu ya utunzi ya kimajaribio.
Mbinu ya utafiti: Mtafiti aliafikia lengo la utafiti kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo mkabala wa ufasili. Mtafiti ameangazia maandiko yenye uhusiano na jinsi riwaya mpya ilivyoichorea hadhira taswira ya jamii husika. Kipengee cha kimajaribio kilichotumika ni matumizi ya simulizi fupi fupi zilizomo katika simulizi kuu. Data ya utafiti ilikusanywa maktabani kutoka katika uchambuzi wa maudhui katika riwaya za Musaleo! (ML) na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji (MMM). Nadharia ya Usasaleo kama ilivyoasisiwa na Jean Baudrillard iliuongoza utafiti katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data.
Matokeo: Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa utaratibu katika utekelezaji wa shughuli mbali mbali uandishi ukiwemo, waweza kuonekana usiofaa lakini hiyo ndiyo taswira kamili ya maisha katika jamii ya kisasa; hayana utaratibu mahususi. Hali ya mparaganyiko imechukua nafasi kubwa ya maisha ya kisasa. Makala imebainisha kuwa jamii inakabiliana na changamoto nyingi. Aidha imeonyesha jinsi jamii yenyewe inavyojimudu kuzitatua.
Mchango wa Kipekee kwa Mujibu wa Nadharia: Mintarafu ya nadharia, mwandishi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya zifuate utaratibu mahususi. Hii ni kwa sababu maisha katika jamii ya kisasa hayana utaratibu wowote.
Downloads
References
Barongo, Y. R. (1980). Neocolonialism and African Politics: A Survey of the Impact of
Neocolonialism on African Political Behavior. New York: Vantage Press.
Baudrillard, J. (1988). Selected Writings. Stanford: Stanford University Press.
Birmingham, D. (1995). The Decolonization of Africa. Ohio: Ohio University Press.
Blum, L. (2004). Stereotypes And Stereotyping: A Moral Analysis Philosophical Papers, [online] Vol. 33. Issue 3. pp 251-289. Available at: <https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1080/05568640409485143> [Accessed 14 January 2020].
Bradford, S. (2007). Diana. London: Penguin Books.
Brown, T. (2008). The Diana Chronicles. New York: Anchor Books.
Jones, H. (1988). Mutiny on the Amistad: The Saga of a Slave Revolt and its Impact on American
Abolition, Law, and Diplomacy. New York: Oxford University Press.
Junor, P. (2005). The Firm: The Troubled Life of the House of Windsor. London: Harper Collins
Publishers.
Lunde, D.T. (1979). Murder and Madness. New York: Norton.
Halliwel, S. (1992). Teaching English in the Primary Classroom. London: Longman.
Malenya, M.M. (2012). Matumizi ya Lugha katika Fasihi Simulizi. Mwanza: Inland Press.
Mutua, J.M., Issa, M., AbdulRahim, T. (2022). Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za K.W. Wamitila. Mwanga wa Lugha 6. 15-26. Eldoret: Moi University Press.
Mutua, J.M., Issa, M. & AbdulRahim, T. (2019). Urejeleomatini katika Uwasilishaji wa Maudhui ya Dhuluma katika Riwaya ya Msichana wa Mbalamwezi (K.W.Wamitila). International Journal of Advanced Research. 7. 303-308. 10.21474/IJAR 01/9038.
Nanjira, D.D. (2010). African Foreign Policy and Diplomacy from Antiquity to the @1st Century. Santa Barbara, CA: Praeger.
Nyabunga, V.A. (2005). Uhakiki wa Bina-damu (2002) na Musaleo! (2004) na K.W. Wamitila.
Tasnifu ya Uzamili; Chuo Kikuu cha Nairobi.
Osagie, I.F. (2000). The Amistad Revolt. Athens & London: University of Georgia Press.
Pakenham, T. (1992). The Scramble for Africa: Whitman's Conquest of the Dark Continent from 1876-1912. New York: Avon.
Rodney, W. (1972). How Europe Underdeveloped Africa. London: Bogle-L'Ouverture Publications.
Smith, S. B. (2007). Diana: The Life of a Troubled Princess. London: Aurum Press Ltd.
Snell, K. (2013). Diana: Her Last Love. London: Andre Deutsch Ltd.
Suret-Canale, J. (1988). Essays on African History: From The Slave Trade To Neo-Colonialism. London: Hurst.
Wacharo, J. (2013). Kanga kama Sajili Maalum ya Kisanii na Mawasiliano. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Moi.
Waller, R. (2014). Kenya: A History Since Independence. London: I.B. Tauris.
Wamitila, K.W. (2004). Musaleo! Nairobi: Vide-Muwa Publishers.
Wamitila, K.W. (2014). Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.
Wilson, T. D. & Gilbert, D. T. (2003). Affective Forecasting. In M. P. Zanna (Ed.), Advances in Experimental Social Psychology, Vol. 35. pp. 345-411. Elsevier Academic Press. https://doi.org/10.1016/S0065-2601(03)01006-2
Yuswanto, F.A. (2015). "Diversity of Existentialism Theory, Patterns and its Reflection in Jurispundence South East Asia Journal Contemporary Business. Economics and Law.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2022
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors retain copyright and grant the journal right of first publication with the work simultaneously licensed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 License that allows others to share the work with an acknowledgment of the work's authorship and initial publication in this journal.